Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhamiaji na maendeleo kumulikwa Geneva

Uhamiaji na maendeleo kumulikwa Geneva

Mkutano kuhusu uhamiaji umeanza mjini Geneva ambapo uhamaiaji na maendeleao unatarajiwa kumulikwa. Mkutano huo ulioko chini ya kundi la kimataifa la uhamiaji GMC, unahusisha mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa  yakiwemo  mfuko wa Umoja wa Mataifa wa idadi ya watu UNFPA na lile la Mpango wa chakula WFP chini ya uenyekiti wa shirika la uhamiaji duniani IOM.Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM na hapa anafafanua zaidi. (SAUTI JUMBE)