UNOCI yalaani shambulio dhidi ya msafara wa wapokonya silaha Ivory Coast:

3 Julai 2013

Mpango wa Umoja wa mataifa wa kulinda amani nchini Ivory Coast Jumanne umelaani vikali shambulio dhidi ya msafara wa wapokonyaji silaha uliokuwa umemmbeba mkuu wa kitaifa wa mpango huu na kutia wito kwamba wote waliohusika na shambulio hilo wafikishwe kwenye mkono wa sheria.

Mpango wa (UNOCI) “umeitaka serikali ya Ivory Coast kuchukua hatua zote ili kubaini waandaaji wa shambulio hilo na kuwachukulia hatua.

Msafara wa uongozi wa kitaifa wa kikosi cha upokonyaji silaha, utulivu na urejeshaji katika maisha ya kawaida (DDR) ulishambuliwa Julai Mosi katika barabara kati ya mji wa wa Ferkessedougou na Kong kaskazini magharibi mwa nchi.

UNOCI inasema mtu mmoja aliuawa na watu wengine watatu kujeruhiwa.