Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka rais Mosri kutopuuza kilio cha wananchi

UM wataka rais Mosri kutopuuza kilio cha wananchi

Ofisi ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu imemtaka rais wa Misri Mohamed Morsi kutoyapuuza madai ya wananchi ambao wanaendesha maandamano wakiulalamikia utawala wake badala imemtaka kuwasilikiliza.

George Njogopa na taarifa kamili.(TAARIFA YA GEORGE)

Kwa mujibu wa msemaji wa tume hiyo ya haki za binadamu Rupert Colville, Ofisi hiyo inaendelea kufuatilia kwa karibu kuhusiana na hali ya mambo nchini humo na kwamba iko nyuma ya wananchi wa Misri  ambao kwa sasa wameingia bara barani kwa siku kadhaa wakiushinikiza utawala wa Mosri kuachia ngazi.

Tume hiyo ya haki za binadamu imesema kuwa rais Mosri hana njia nyingine ya mkata mbali ya kusiliza kilio cha wananchi ambao wanazidi kumiminika mitaani kwa maandamano ya amani.

Misri imekuwa katika hali tete, tangu kulipoasisiwa serikali ya mpito baada ya kupinduliwa na serikali ya kidikta ya Hosni Mubarak miaka miwili iliyopita kufuatia wimbi la mageuzi lilizikumba nchi kadhaa za kiarabu.

Mamia ya waandamanaji wamekuwa wakijitokeza katika miji mbalimbali wakishinikiza kuondoka madarakani kwa rais Morsi kwa madai kuwa ameshinda kazi.

Kama sehemu ya koongeza shinikizo hapo jana jeshi lilitoa muda wa saa 48 kwa rais Morsi kujiuzulu zingatio ambalo hata hivyo limekataliwa na kiongozi huyo.