Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wako katika hatari kubwa ya ukatili unaohusiana na silaha:

Wanawake wako katika hatari kubwa ya ukatili unaohusiana na silaha:

Wanawake ndio idadi kubwa ya waathirika wanaouawa a, kujeruhiwa au kukabiliwa na vitisho vya silaha majumbani kwa mujibu wa utafiti wa karibuni wa silaha ndogo ndogo duniani.Takwimu kutoka mataifa 111 zinaonyesha kwamba wanawake takribani 66,000 wanauawa kikatili kila mwaka kwa silaha huku idadi kubwa ya vifo ikitokea majumbani na vikitekelezwa na wepenzi wao wa sasa au wa zamani.

Utafiti huo ambao umechapishwa na tasisi ya Uswis mjiniGenevaimebaini kwamba usawa wa kijinsia,uvumilivu na utamaduni wa kukubali matumizi ya ukatili dhidi ya wanawake na mtazamo wa mfumo dume ambao unakumbatia umiliki wa silaha, vimeungana kuunda mazingira ambayo yanmuweka mwanamke katika hatari kubwa ya ukatili inaohusisha silaha.

Utafiti unasema hadi asilimia 60 naya mauaji ya kikatili yanafanywa kwa silaha na vingi vinatokea katika nchi ambazo haziko katika hali ya vita. Bi Anna Alvazzi del Frate ni mkurugenzi wa utafiti kuhusu silaha ndogondogo.

(SAUTI YA ANNA ALVAZZI)

“Tumehesabu karibu watu 526,000 hufa kikatili kila mwaka, lakini asilimia 10 tuu ndio katika mazingira ya vita, wakati vita baiana ya mataifa vikipungua tangu mwaka 2004. Hii inaonyesha kwamba idadi kubwa ya vifo vya kikatili vinatokea nje ya vita au uwanja wa mapambano. Matokeo ya utafiti wetu yanaainisha kwamba hatari ya mpenzi kufanya ukatili kwa kutumia silaha ni kubwa kwa ujumla. Na hatari imeongezwa na uwepo wa silaha nyumbani na kazi zinazotumia silaha. Ingawa wamiliki wakubwa wa silaha ni wnaume, wahanga wakubwa ukatili wa nyumbani ni wanawake.”

Utafiti unasema raia wanahodhi karibu asilimia 75 ya takribani silaha milioni 875 zinazomilikiwa duniani , huku vikosi vya serikali vya ulinzi na usalama ninamiliki chini ya robo ya akiba ya silaha duniani