UNHCR yakaribisha hatua ya serikali ya Pakistan kuendelea kuwapa hadhi wakimbizi wa Afghanistan

2 Julai 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UHNCR limetoa taarifa likikaribisha hatua ya serikali ya Pakistan ya kurudia tena ahadi yake ya kuendelea kutoa hifadhi ya ulinzi kwa zaidi wa wakimbizi milioni 1.6 kutoka Afghanistan.Waziri mpya wa Pakistan juu ya masula ya serikali na mstari wa mbele Abdul Qadir Baloch, amekutana na ujumbe wa pande tatu, serikali ya Afghanistan, UNHCR na Pakistan yenyewe na kutoa ahadi kwamba wakimbizi wa Afghanistan wataongezewa muhula mwingine kuendelea kutumia kadi ambazo zinaatambulika “ uthibitisho wa kuandikishwa”.

Pakistan inaendelea kusalia moja ya nchi yenye idadi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani na tangu mwaka 1979 imekuwa ikiwahifadhi wakimbizi wa Afghanistan na Soviet kwa hisani tu.

Ikijadilia hali hiyo, UNHCR imesema kuwa hiyo ni ya kuu