Amri ya rais Obama ya kupambana na uwindaji haramu yapokelewa na kamati husika

2 Julai 2013

Kamati inayohusika na vita dhidi ya biashara ya wanyamapori walio kwenye hatari ya kuangamia imekaribisha amri iliyotolewa na rais wa Marekani Barack Obama ya kutaka kuchukuliwa kwa hatua za kimataifa za kuzuia biashara haramu ya wanyamapori . Alice Kariuki na taarifa zaidi.(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Amri hiyo inahusu kubuniwa kwa jopo kazi la rais kuhusu usafirishaji haramu wa wanyapori litakalosimamiwa na waziri wa mambo ya kigeni kwa ushirikiano na Waziri wa masuala ya ndani na mkuu wa sheria ambao wanaripoti kwa rais kupitia kwa mshauri kuhusu masuala ya ulinzi. Amri hii ya rais Obama inatuma ujumbe mkubwa wa kimataidfa wa katska uhalifu dhidi ya wanyamapori kuchukuliwa kuwa uhalifu ulio mkubwa. Uwindaji haramu wa wanyamapori umepanuka kutoka kwa shughuli iliyokuwa ndogo hadi viwango vya juu vinavyohusu shughuli zilizopangwa na makundi ya uhalifu yaliyojihami . Kuendelea kuwpo ka wanayapori kama vile ndovu, kiboko, sokwe mtu, mnynagumi kuna manufaa ya kuchumi , kijamii namazingira wakiwa na umuhimu mkuwa kwa mataifa yote.