Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yahamisha shughuli zake kutoka kusini mwa Tunisia kwenda mijini

UNHCR yahamisha shughuli zake kutoka kusini mwa Tunisia kwenda mijini

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa limekamilisha shughuli za utoaji huduma kwa watu kutoka kambi ya Choucha iliyo kusini mwa Tunisia na kwenda  kwa maeneo yaliyo karibu na miji. Hadi mwishoni mwa mwezi Juni zaidi ya wakimbizi 600 walikuwa wakiishi kwenye miji iliyo kusini nchini Tunisia ya Ben Gardane na Medenine.

Idadi ya watu kwenye kambi ya Choucha imepungua tangu mwaka 2011 na kuchangia UNHCR kuhamishia huduma zake mijini . Kufungwa wa kambi hiyo kumeungwa mkono na utawala wa Tunisia ambao umeahidi kutoa makao ya muda kwa wakimbizi 250 ambao hawateweza kupata makao nchi zingine.

Shughuli ya kuhamisha wakimbizi kwenda kwa nchi walikopewa makoa kutoka kambi ya Choucha kupitia kwa mpango uliong’oa nanga kufuatia kuhama kwa watu kutoka nchiniLibyanwaka 2011 ulishika kasi kati kati ya mwaka uliopita. Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR .

(SAUTI YA ADRIAN)