Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID imejikita katika kumaliza mzozo Darfur

UNAMID imejikita katika kumaliza mzozo Darfur

Ikiwa ni takribani muongo mmoja wa mapigano katika jimbo la Darfur nchini Sudan kati ya serikali na waasi imeelezwa kuwa mazungumzo baina ya pande zinazokinzana ndio muarubaini mzozo huo uliodumu kwa muda mrefu.

Katika mahojiano maalum na mwandishi wa idhaa ya kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa Asumpta Massoi, kaimu kamanda wa kikosi cha UNAMID Meja Jenerali Wynjones Mathew Kisamba amesema pamoja na mazungumzo, kufanya kazi kwa pamoja kutamaliza mzizi wa fitina na hapa anaanza kueleza lini alianza kufanya kazi.

(SAUTI MEJA JENERALI KISAMBA)