Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mawaziri wataka juhudi zaidi kulinda dunia dhidi ya nyuklia

Mawaziri wataka juhudi zaidi kulinda dunia dhidi ya nyuklia

Wakati mkutano wa kimataifa kuhusu usalama wa nyuklia ukiwa umeanza mjini Vienna Austria mawaziri husika katika mkutano huo wamesema licha ya hatua zilizopigwa katika usalama dhidi ya nyuklia katika miaka ya hivi karibuni, hatua zaidi zinahitajika kulinda dunia dhidi ya tishio la ugaidi wa nyukilia na vitendo vyote vinavyohusisha nyukilia.

Tamko la mawaziri hao liliamuliwa katika kikao kilichohusisha mawaziri 34 na wawakilishi wengine akiwamo rais wa mkutano, ambapo sehemu ya tamko hilo inazitaka nchi kudumisha usalama dhidi ya nyuklia ikiwa ni pamoja na ulinzi dhahiri kwa nyenzo zote za kemikali hizo, mionzi , matumizi na usafiri wake na kulinda habari nyeti na kudumisha mifumo ya usalama , kusimamia kwa kutathimini na ufanisi.

Mawaziri hao walikaribisha kazi ya IAEA na kutambua juhudi zake katika kukuza uelewa wa kukua kwa tishio la mashambulizi ya kimtandao na atahri zake juu ya uwezo wa usalama wa nyuklia.

Mkutano huu unaohusisha washiriki 1300 wa wanachama 159 wa shirika la kimataifa la nguvu za atomiki IAEA utaainisha juhudi za sasa na za zamani za usalama wa nyukilia na namna changamoto za siku za usoni zinaweza kutatuliwa ili kuhjakikisha usalama endelevu wa nyuklia duniani.