Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya, Global Fund na UNAIDS zashirikiana kupambana na HIV, TB na malaria

Kenya, Global Fund na UNAIDS zashirikiana kupambana na HIV, TB na malaria

Katika ziara ya pamoja, mkuu wa kitengo cha masuala ya HIV na UKIMWI katika Umoja wa Mataifa, Michel Sidibe na mkuu wa hazina ya kimataifa ya kupambana na UKIMWI, kifua kikuu na malaria, Mark Dybul, wameonyesha ishara ya ushirikiano wa dhati katika kupiga vita magonjwa ya kuambukiza, yakiwemo HIV na kifua kikuu.

Wakuu hao wa UNAIDS na Global Fund, wamekutana na viongozi wa serikali mpya nchini Kenya pamoja na mashirika ya umma na wadau wengine, na kutia saini makubaliano ya ufadhili mpya, na hivyo kuashiria kujitolea kwa ushirikiano mpya.

Ufadhili huo wenye thamani ya dola milioni 27 za kimarekani, utasaidia programu zinazotekelezwa kwa pamoja na wizara ya fedha nchini Kenya, na shirika la AMREF, ambalo limekuwa likijitahidi kuboresha afya ya jamii za Afrika kwa zaidi ya miaka 50.

Fedha hizo zitafadhili programu za kuboresha upimaji na matibabu ya kifua kikuu, kupunguza kucheleweshwa kwa upimaji miongoni mwa watu walio hatarini na kutoa msaada wa lishe kwa wagonjwa wa kifua kikuu. Zitawasaidia pia watu waloambukiwa