Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malengo ya Maendeleo ya Milenia yapiga hatua kubwa: Ban

Malengo ya Maendeleo ya Milenia yapiga hatua kubwa: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa  Mataifa Ban Ki Moon amesema wakati ukomo wa maendeleo ya milenia mwaka 2015 unapokaribia ni wazi kwamba utekelezaji wa malengo hayo unaridhisha licha ya changamoto zilizosalia.(Taarifa zaidi na Geroge Njogopa)

Akizindua ripoti kuhusu malengo ya maendekeo ya mallenia mjiniGeneva, Ban Ki-moon amesema kuwa kumekuwa hatua kubwa zilizopigwa na kutolea mfano lengo mojawapo la upunguzwaji wa tatizo la umaskini

Katika hiloamesema kuwa, kiwango cha watu waliokuwa wakiishi kwenye hali ya umaskini sasa kimepungua na kufukia nusu na kwamba zaidi ya watu bilioni 2.1 sasa wanazo fursa za kuwa na vyanzo majisafina salama.

SAUTI YA BAN:

‘’Tumepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya malaria na kifua kikuu , hii inaonyesha kwamba nguvu za pamoja za serikali, jumuiya ya kimataifa , jumuiya za kijamii na sekta binafsizinaweza kuleta mabadiliko makubwa. Hata hivyo ripoti pia imeelezea changamoto kubwa, mazingira endelevu yako katika tisho kubwa, watoto 19 wa chini ya umri wa miaka mitano wanakufa kila siku, wengi wao kwa magonjwa yanayoweza kuzuilika. Wanawake wanaendelea kunyimwa haki sawa za kushiki katika maamuzi kwenye ngazo zote. Lazima tuzidishe juhudi zetu hususani kushughulikia tofauti zilizoto katika kanda na makundi tofauti ya kijamii."