Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kimataifa kuhusu usalama wa nyuklia waanza Vienna:IAEA

Mkutano wa kimataifa kuhusu usalama wa nyuklia waanza Vienna:IAEA

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA , Yukiya Amano, leo amefungua mkutano wa kimataifa wa usalama wa nyuklia mjini Vienna kwenye makao makuu ya IAEA.

Mkutano huo wa siku tano umewaleta pamoja washiriki 1300, wakiwemo mawaziri 34 kutoka nchi 120 na mashirika ya20 ya kimataifa na kikanda.

Mkutano huo unatarajiwa kutoa fursa ya kimataifa kwa mawaziri, watunga sera na maafisa wa ngazi za juu wa serikali mbalimbali kuchangia mawazo kuhusu mustakhbali wa muelekeo wa siku za usoni na masuala ya kuyapa kipaumbele ili kuimarisha suala la usalama wa nyuklia.