Mpango wa Marekani na Urusi ni ya mzozo wa Syria: Ban

1 Julai 2013

Juhudi za Marekani na Urusi kuzileta pamoja pande mbili zinazopigana kwenye meza ya mazungumzo ndio suluhu ya kudumu itakayoleta amani na kuokaoa maoisha, amesema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon.

Akongea mjini Geneva Bwana Ban amesema ingawa kuna hatua zilizofikiwa katika mkutano wa kimataifa kuhusu Syria kumekuwa na vikwazo ikiwamo ushiriki wa Iran na Saudi Arabia.

Amesema ilikuwa muhimu kwamba upinzani uhudhurie mkutano kama kundi lililoungana na ujumbe wa serikali uwezeshwe kujadili.

“Watu wa Syria wanahitaji amani na matumaini. Kinyume na hayo wanachoona ni vifo juu ya vifo. Wanachosikia ni mazungumzo kila wakati . Watu wanakufa. Moto wa Syria unaendela kusambaa. Unaweza kukumba ukanda mzima. Tunatarajia ujumbe hususani kutoka upinzani watatuam wawakilishi wao wakiwa wameungana na madhubuti. Tunatarajia pia ujumbe wa serikali utawezeshwa vilivyo ili kushiriki kikamilifu katika mazungumzo kwa ushirika na mjumbe maalum Lakhdar Brahimi. Kuna swala lingine la wigo wa kushiriki kwa Iran na Saudi Arabia. Nchi wanachama hawajakubaliana kama sauti zao zinahitaji kusikika na namna gain..”