Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yawasilisha msaada kwa wakimbizi 26,000:Syria

IOM yawasilisha msaada kwa wakimbizi 26,000:Syria

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanza kufikisha msaada kwa wakimbizi wa Syria 26,000 familia zinazowahifadhi na familia za Kilebanon zinazorejea huko Kusini mwa Lebanon. Katika mahojiano na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa ,msemaji wa IOM Jumbe OmariJumbe anasema mapigano kati ya jeshi la serikali ya Lebanon na waasi wanaomuunga mkono kiongozi wa kidini Salafi , yalikwamisha operesheni za misaada za IOM lakini sasa operesheni hizo zimeanza.

Kadhalika Jumbe anatoa wito wa kumaliza mgogoro wa Syria kwa suluhu ya kisiasa lakini kwanza anaazna kwa kueleza namna misaada kwa wakimbizi hao inavyotolewa.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)