Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya chanjo ya polio Burundi baada ya tishio kutoka DRC

Kampeni ya chanjo ya polio Burundi baada ya tishio kutoka DRC

Serikali ya Burundi  kwa ushirikiano na  shirika la Afya Duniani WHO wameanzisha kampeni kabambe  dhidi ya ugonjwa wa kupooza wa polio.

Hii ni baada ya Burundi kujikuta  katika kitisho kikubwa cha kuvamiwa na maradhi hayo baada ya nchi  jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuonyesha dalili za Polio katika maeneo ya  kusini na mashariki mwa nchi hiyo.

Watoto zaidi  ya Milioni 1 na Laki 2 wanahusishwa na kampeni ambayo pia  Shirika la WHO limepania kuineza katika maeneo mbalimbali ya DR Congo.

Kutoka Bujumbura, Muandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani KIBUGA ametuandalia makala hii.

(Makala ya Kibuga Ramadhani)