Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuuawa kwa wakimbizi wa ndani wawili Myanmar kwa itia hofu: UNHCR

Kuuawa kwa wakimbizi wa ndani wawili Myanmar kwa itia hofu: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linatiwa hofu na tukio la ghasia lililofanyika Alhamisi Mashariki mwa jimbo la Myanmar la Rakhine na kusababisha vifo vya wakimbizi wa ndani wawili.

Watu wengine sita walijeruhiwa katika tukio hilo wakiwemo watoto wawili. UNHCR imetoa wito wa kufanyika uchunguzi haraka wa tukio hilo.Shirika hilo pia limeitaka serikali kushughulikia suala hilo kwa njia ya amani na utulivu ili kuepuka kupotea kwa maisha ya watu na kuchochea ghasia zaidi.