Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya wakimbizi wa ndani CAR ingali tete: WFP

Hali ya wakimbizi wa ndani CAR ingali tete: WFP

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP limesema hali ya wakimbizi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati bado ni tete, na kwamba hali hii huenda ikaathiri vibaya mno kampeni ya sasa ya kilimo ya mwaka 2013 hadi 2014. Joseph Msami na maelezo zaidi

(TAARIFA YA JOSEPH MSAMI)

Kwa mujibu wa tathmini ilofanywa baada ya timu ya WFP kuzuru maeneo 60 katika kata 8 kati ya 11, kaya nyingi zimepoteza maghala ya chakula, vifaa vya ukulima, mbegu, mifugo na mapato kutokana na uporaji na mzozo ambao umeendelea kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa WFP, ingawa masoko yameanza kufunguliwa tena kwa kiwango kidogo, bado kuna uhaba wa bidhaa za chakula na bei zimeongezeka. Uwezo wa watu kumudu kununua bidhaa pia umepungua, kwani wengi wao wamepoteza tegemeo lao la riziki, na sasa watu walio wanyonge zaidi sasa hula mara mora tu kwa siku, huku aina za mlo zikipungua. Kwa mujibu wa tathmini hiyo, ikwa msaada hautatolewa kwa watu hao waloathiriwa na migogoro, msimu ujao wa uhaba wa chakula utawaathiri na kuwaweka katika hatari ya utapiamlo. WFP inapanga kuwasaidia zaidi ya watu 127,000 tokea sasa hadi mwezi Agosti. Msemaji wa WFP, Elisabeth Byrs anaeleza zaidi

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)