Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi 10 zajitolea kutokomeza malaria Amerika ya Kati na Karibea

Nchi 10 zajitolea kutokomeza malaria Amerika ya Kati na Karibea

Nchi kumi za Amerika ya Kati na eneo la Karibea zimejiunga kwenye mkakati wa kikanda unaolenga kutokomeza ugonjwa wa malaria ifikapo mwaka 2020, kwa msaada wa hazina ya kimataifa ya kupiga vita UKIMWI, kifua kikuu na malaria, Global Fund.Haya yametangazwa kwenye mkutano wa kikanda wa mawaziri wa afya kutoka Amerika ya Kati na eneo la Karibea, na unanuia kuunganisha na kuongeza kasi ya juhudi za kutokomeza malaria katika nchi za Mexico, Belize, Guatemala, Honduras, El Salvador, Nicaragua, Costa Rica, Panama, Haiti na Jamhuri ya Dominika.

Hazina ya Global Fund ambayo kwa sasa inasaidia kufadhili vita dhidi ya malaria Nicaragua, Honduras, Guatemala, Jamhuri ya Dominika na Haiti, imetenga dola milioni 10 kwa ajili ya mkakati huo wa kikanda.