Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR kusaidia wakimbizi wa Mali kupiga kura ugenini

UNHCR kusaidia wakimbizi wa Mali kupiga kura ugenini

Ukiwa umesalia mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa Rais nchiniMalihapo Julai 28, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linaimarisha shughuli za kusaidia nchi jirani kukabiliana na upigaji kura wa wakimbizi waMalikatika nchi hizo.Burkina Faso, Niger na Mauritania kwa pamoja zinahifadhi wakimbizi 175,000 waMaliwaliongia kutokana na machafuko ya karibuni. Wakimbizi watakaoweza kupiga kura ukimbizini ni wale ambao tayari wameshajiandikisha wakati wa sensa iliyofanyika nchiniMalimwaka 2010. UNHCR inawapa wakimbizi taarifa ya hakiyaoya kushiriki kwenye uchaguzi na pia inawasaidia usafiri kwenda kupiga kura vituoni. Upigaji kura kwa wakimbizi hao utakuwa ni wa hiyari na wameshaarifiwa ipasavyo.