Haki za binadamu njia panda wakati machafuko yakishika kasi Iraq

27 Juni 2013

Licha ya baadhi ya hatua kupigwa , haki za binadamu nchini Iraq ziko katika tishio kubwa kutokana na ongezeko la machafuko , imesema ripoti ya haki za binadamu iliyotolewa leo. George Njogopa na ripoti kamili.(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 Ripoti hiyo iliyochapishwa na ofisi ya tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa kwa ajli ya Iraq UNAMI imeangazia hali jumla ya haki za binadamu nchini humo kwa kipindi cha Julai mosi hadi disemba 31 mwaka uliopita wa 2012.

Imetilia shaka juu ya kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu vinavyoenda sambamba na matumizi ya silaha ambako imeeleza kuwa kiasi cha raia 3,238 waliuwawa na wengine 10,379 wamejeruhiwa katika kipindi cha mwaka uliopita.

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchino humo Martin Kobler amesema kuwa ongezeko hilo linatoa picha kwamba kuna kazi kubwa inayopaswa kufanywa sasa.

Kwa upande mwingine amewatolewa mwito viongozi wa Iraq kuanzisha duru la majadiliano na kusuma mbele sera zinazohimiza amani na mshikamano.