Miaka 20 baada ya makubaliano ya Vienna bado ukatili waendelea: Pillay

27 Juni 2013

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema licha ya mafanikio makubwa  tangu kuanza kutekelezwa kwa makubaliano kuhusu haki za binadamu mjini Viennamwaka 1993, bado makubaliano hayo yamekabiliwa na changamoto nyingi. Grace Kaneiya na ripoti zaidi.

(Taariaf ya grace)

Akifungua mkutano wa siku mbili hukoAustria wa kuadhimisha miaka 20 tangu makubaliano yaVienna kuhusu hali ya kibinadamu mwaka 1993, Bi. Pillay amesema hatua kubwa zimepigwa ndani ya kipindi hicho licha ya kwamba bado kuna mengi ambayo hayajatekelezwa. Amesema miaka ishirini iliyopita watoto walikuwa wakipigwa risasi kwenye mitaa yaSarajevo hukoBosnia, lakini hata leo bado yapo makundi yanalia yakitafuta usaidizi huko DRC,Somalia naSyria.

 (SAUTI YA PILLAY)

 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson naye akasema inavyoonekana sasa ghasia na ukatili vimezoeleka duniani.

(SAUTI YA ELIASSON)

 Viongozi hao wametaka jamii ya kimataifa kusaidia wale wanaokumbana na ukiukwaji wa haki za binadamu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud