Watoto wanaofanya kazi katika sekta ya uvuvi walindwe:FAO/ ILO

Watoto wanaofanya kazi katika sekta ya uvuvi walindwe:FAO/ ILO

Serikali zimetakiwa kuchukua hatua madhubuti za kuwalinda watoto kutokana na madhara ya kazi katika sekta za uvuvi na ufugaji wa viumbe vya majini . Kauli hiyo imetolewa na shirika la kilimo na chakula FAO na lile la kazi ILO. Jason Nyakundi na taarifa zaidi(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Watoto wengi wanapitia hali ngumu  ya kufanya kazi inayowaathiri kiafya na uwezo wao wa kujifunza kulingana na ripoti iliyochapishwa kw pamoja na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa likiwemo la kilimo na mazao FAO na  la kazi ILO.

Ripoti hiyo inasema kuwa kila nchi imetia sahihi makubaliano ya kimataifa ya kulinda watoto lakini hazijafanya makubalino hayo kuwa sheria.

Ripoti hiyo inasema kuwa watoto wanaingia kwenye mashimo yenye vina kirefu usiku wakifanya kazi muda mrefu kwenye mazingira yaliyo mabaya wakikabiliwa na hatari ya kuambukizwa magonjwa au kupata majera kutokana na vifaa wanavyotumia.

Watoto wasichana wanaofanya kazi kwenye viwanda vya samaki wanakabiliwa na hatari ya kudhulumiwa kimapenzi.  Mkurugenzi mkuu katika kitengo cha uvuvi kwenye Shirika la FAO Árni M. Mathiesen anasema kuwa ajirakamahizi hazikubaliki kuwa zinaathiri afya ya watoto.