Akizungumzia kuchanuka kwa Afrika Ban pia akumbuka afya ya Mandela

27 Juni 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mmoja wa majabali ya Afrika kwa karne ya 20 Mzee Nelson Mandela yu mahututi hospitali na kusema kuwa mawazo na sala za kila mmoja zinaelekezwa kwake, familia yake, watu wa Afrika ya Kusini na dunia nzima ambao wameguswa na ujasiri na maisha yake. Flora Nducha anaripoti(RIPOTI YA FLORA NDUCHA)

Ban ameyasema hayo wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya tangu kuanzishwa Muungano wa Afrika zamani OAU na sasa AU, iliyofanyika hapa New York Jumatano jioni.

Ban amesema anaelewa kuwa bado kuna changamoto kubwa zinazolikabili bara la Afrika lakini kwa ujumla matumaini na matarajio ya mafanikio yako bayana.

Amesema Afrika ni bara lililo mbioni, amani imepatikana katika nchi nyingi, umasikini uliokithiri unapungua, kipato kinaongezeka na kuna hatua kubwa ya katika kukabili n maradhi yanaotua.

Ameongeza kuwa watu wengi Afrika hivi sasa wanapata fursa za kujiendeleza na wawekezaji wa kimataifa wanajitokeza hivyo Arika inajiandikia historia.

Pamoja na mafanikio yote hayo Ban amesema ili kufikia malengo Afrika inahitaji kutatua chanzo cha migogoro.