Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNECE yapitisha mipango mipya

UNECE yapitisha mipango mipya

Shirika la Umoja wa Mataifa la UNECE limefaulu kupitisha agenda muhimu ambayo inatoa mwongozo na kanuni ya usafi wa hydrogen na mitambo inayotumia nishati za kati.

Miongozo hiyo inaainisha mambo yanayopaswa kuzingatiwa ili ikiepusha athari zinazoweza kujitokeza wakati kunapofanyika shughuli zikiwemo zile zinazotumia umeme.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema kuwa kupitishwa kwa azimio hilo kutasaidia kusukuma mbele teknolojia na wakati huo huo kukabiliana na hali ya uchafuzi wa anga.