Msimu wa kiangazi waleta furaha kwa watoto wa kipalestina: UNRWA-EU

Msimu wa kiangazi waleta furaha kwa watoto wa kipalestina: UNRWA-EU

Kwa mwaka wa tatu mfululizo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya, EU wamekuwa wakihakikisha msimu wa kiangazi unakuwa wa furaha kwa watoto wakimbizi wa Kipalestina wapatao Elfu Sita kwenye Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan.

Katika kipindi cha takribani cha kuanzia tarehe 23 Juni hadi tarehe Nne Julai watoto hujumuika kwenye michezo mbali mbali inayowapatia pia stadi, licha ya machungu ya maisha wanayokumbana nayo.

Mathalani ushairi, michezo ya kuigiza na muziki ikiwa na mchanganyiko wa tamaduni ikiwezo za Ulaya ambapo Mohammed Assaf aliibuka mshindi wa shindano la nyota bora wa kiarabu na kutunikiwa cheti na kuteuliwa balozi mwema wa UNRWA. Filipo Grandi ni mkuu wa UNRWA.

(SAUTI YA GRANDI)

“Tunaye mwana wa Gaza, mkimbizi wa kipalestina ambaye ni balozi wetu wa kwanza kabisa wa kwanza kabisa. Nilimweleza Mohammed mapema kuwa nimekuwa nikipokea katika eneo hili wakuu wengi wa nchi na mawaziri wakuu lakini sijawahi kusikia furaha na shauku kubwa kama leo.”