UN Women yazindua wito wa kuhakikisha usawa wa kijinsia unafanikiwa

26 Juni 2013

Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachiohusika na masuala ya wanawake UN-Women kimezindua wito maalumu wa kimataifa kuhakikisha sababu zinazokwamisha mafanikio ya usawa wa kijinsia , haki za wanawake na kuwawezesha wanawake zinatokomezwa kwa kuchukuliwa hatua madhubuti ambazo zitawawezesha wanawake na wasichana waishii kama raia sawa na wengine popote.Katika waraka uliotolewa leo UN-Women inatoa mwongozo kuhusu sera ambazo ni za lazima katika kukumbatioa mabadiliko ya kudumu ili wanawake na wasichana wahakikishiwe usawa kote duniani.

Wito huo umekuja wakati kukiwa na mjadala wa kimataifa kuhusu wosia na hatuza zitakazofuata baada ya malengo ya maendeleo ya milenia hapo 2015, ambayo yamekuwa msitari wa mbele kupunguza umasikini tangu mwaka 2000.

Waraka huo wa UN women unasisitiza kwamba ajenda ya baada ya 2015 ijikite katika kuendeleza mafanikio ya malengo ya milenia na kuepuka mapungufu yake.

Unasisitiza kwamba kwa kutambua haki za wanawake ni muhimu kushughulikia chanzo cha kutokuwepo usawa wa kijinsia kama vile ukatili dhidi ya wanawake, kazi za bila malipo, kutokuweza kumuliki mali,kutokuwepo usawa wa ushiriki katika kufanya maamuzi kwenye sekta binafsi na za umma.

UN-women inapendekeza malengo matatu ambayo kuwa huru na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. Usawa wa kijinsia katika majukumu, na usawa wa kijinsia katika ngazi ya maamuzi.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud