Ibua mbinu kuboresha afya na si kubuni dawa mpya za kulevya: UNODC

26 Juni 2013

Fanya afya kipaumbele chako na siyo madawa ya kulevya, ni ujumbe mahsusi wa Umoja wa Mataifa hii leo ambayo ni siku ya kimataifa dhidi ya matumizi na usafirishaji wa madawa ya kulevya. Ripoti ya Flora Nducha inafafanua zaidi.(Ripoti ya Flora)

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti madawa ya kulevya na uhalifu UNODC inaeleza bayana kuwa matumizi ya madawa yanaharibu afya na ustawi wa binadamu huku ikionyesha wasiwasi kutokana na kuibuka kwa tatizo jipya la ongezeko la mahitaji ya madawa yasiyo chini ya udhibiti wa kimataifa ambayo huchanganywa na watumiaji hulewa, madawa ambayo ni tofauti na yale yaliyozoeleka ambayo ni Cocaine, Heroine na bangi.

Mkuu wa maabara ya kisayansi ya UNODC Justice Tettey anasema kuwa madawa hayo yanauzwa kihalali kabisa lakini mchanganyiko wake hujipatia majina ya mtaani kama vile SPICE au Meow-Meow na vijana kudhani kuwa hayana madhara.

(SAUTI YA Tettey)

Fatma Musa Juma ni mmiliki wa moja ya makazi ya kusaidia watumiaji wa madawa ya kulevya huko Tanzania Zanzibar kurejea katika maisha ya kawaida. Je vijana hupataje fedha za kununua madawa hayo?

(SAUTI YA FATMA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud