Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM wazitaka serikali kuwasaidia wahanga wa utesaji na familia zao:

Wataalamu wa UM wazitaka serikali kuwasaidia wahanga wa utesaji na familia zao:

Serikali zimeaswa kuwa ni lazima zijitahidi kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha kwamba wahanga wa utesaji na familia zao wanapata msaada na unaostahili kutokana na madhila waliyotapata .

Kauli hiyo imetolewa na wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuwaunga mkono waathirika wa utesaji ambayo kila mwaka hufanyika Juni 26.

Wataalamu hao wameainisha ukweli kwamba waathirika hao mara nyingi hukabiliwa na changamoto ya kupata msaada wa kimwili, kiakili, haki na fidia ambazo wanastahili. Wameongeza kuwa kwa bahati mbaya utesaji unaendelea katika nchi mbalimbali na hali hiyo ni lazima ipatiwe ufumbuzi.