Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakutana Cairo kujadilia mpango wa kuendeleza nchi za Kiarabu

Wakutana Cairo kujadilia mpango wa kuendeleza nchi za Kiarabu

Viongozi wa kiserikali, mashirika ya kiraia pamoja na wataalamu kutoka sehemu mbalimbali duniani wamerejea tena Cairo nchini Misri, kwa ajili ya kutathmini mpango ulisisiwa nchini humo mnamo mwaka 1994 ambao uliweka maazimio yanayohusu idadi ya watu kwa nchi za kiarabu na agenda ya maendeleo kuelekea mwaka 2014. Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA, Dr. Babatunde Osotimehin,amesema kuwa ni jambo la furaha kwa wajumbe kukusanyika pahala ambapo miaka 20 iliyopita mpango huo uliasisiwa.

Kongamanohiloambalo linafanyika chini ya kauli mbiu isemayo “maendeleo na mabadiliko ya idadi ya watu  katika kuubadilisha ulimwengu wa kiarabu” limewaleta pamoja zaidi ya wajumbe 350 kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo,Waziri wa afya wa Misri Dr.Mohammed Moustafa, alihimiza juu ya haja ya kuzingatia yale yaliyoanishwa kwenye mpango huo wa maendeleo.