Watunga sera warahisishe uhamiaji na si kuzuia: UM waelezwa

25 Juni 2013

Uhamiaji ulikuwepo na utaendelea kuwepo na una nafasi kubwa katika maendeleo ya nchi yoyote ile duniani hivyo ni wajibu wa watunga sera kuweka mazingira ya kurahisisha uhamiaji badala ya kuweka vizingiti. Hiyo ilikuwa sehemu ya kauli ya Douglas Massey kutoka Chuo Kikuu cha Pricetown kwenye kikao cha ngazi ya juu cha Umoja wa Mataifa mjiniNew York, Marekani kinachoandaa mashauriano ya pili kuhusu uhamiaji wa kimataifa na maendeleo kitakachofanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Bwana Douglasa meonyesha mshangao wake wa mataifa kuweka majeshi mpakani mwao kuzuia wahamiaji akieleza kuwa sera za namna hiyo zinazuia hata wale wanaotaka kurejea nyumbani kushindwa kwa hofu ya kukamatwa. Amesema utandawazi wenyewe ni kichocheo tosha cha uhamiaji na hakuna nchi iliyopitia awamu zote za maendeleo kuanzia ile ya awali hadi ya kisasa bila kutumia wahamiaji akitaja kuwa hata katika karne ya 19 na 20 wakazi wa barani Ulaya walihamia siyo tu miji mikubwa barani humo bali pia mabara mengine kutokana na kukua kwa masoko na biashara. Hivyo basi akatoa somo kwa watunga sera.

(SAUTI YA MASSEY)

 

“Mchakato wa maendeleo ya kiuchumi huibua wahamiaji, na changamoto ya sera kwa watunga sera kwa nchi zinazoendelea na zilizoendelea ni kutunga sera siyo ya kuzuia uhamiaji ambao unaweza kutokea bali kushughulikia kwa uzuri ili iwe na maslahi kwa pande zote, badala ya kuweka vizingiti na hivyo iwe na madhara kidogo na faida zaidi kwa pande zote zinazotoa na zinazopokea wahamiaji. Hii ndiyo changamoto ya msingi kwa karne hii ya 21.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter