Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM na Tunisia zachapisha utafiti mpya kuhusu usafirishaji haramu wa binadamu

IOM na Tunisia zachapisha utafiti mpya kuhusu usafirishaji haramu wa binadamu

Shirika la Kimataifa la uhamiaji IOM limechapisha utafiti wake unaoangazia hali usafirishaji haramu wa watu nchiniTunisia. Utafiti huo ambao umefanywa kwa pamoja kati ya IOM na serikali ya Tunisia unaonyesha kuwa vijana wengi nchini humo wapo hatarini kusafirishwa katika mataifa ya nje. Waendeshaji wa vitendo hivyo wanaripotiwa kutoa ahadi za uongo kwa vijana hao ikiwemo kuwaahidi kuwatafutia kazi ambazo zinalipa vizuri.   Ripoti hiyo imesema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa  la matumizi ya mitandao ya kijamii ikiwemo internet kwa ajili ya kuwarubuni vijana hao ambao baadaye wanaishia kutumikishwa kwenye shughuli ngumu na ujira mdogo Tunisia.