Watoto ndio wajenzi na viashiria vya jamii zenye afya na endelevu: UNICEF

24 Juni 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema mwaka mmoja baada ya mkutano wa Rio+20 kuhusu mustakhbali tunaohitaji, ni dhahiri shahiri kuwa matokeo ya mkutano huo yatategema vile ambavyo watoto watawekwa kuwa kitovu cha ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015. George Njogopa na taarifa zaidi. (RIPOTI YA GEORGE)

UNICEF katika taarifa yake hiyo mpya yenye kichwa cha habari “Maendeleo endelevu huanza na kuishia kwa kuzingatia usalama, afya, na watoto walioelimishwa vyema, imebainisha maeneo muhimu matatu ambayo imeyatajakamamsingi wa kufikia shabaha ya kukuza ustawi kwa watoto.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni pamoja na kuwasuma watoto kusonga mbele, ikielezwa kuwa kwa kufanya hivyo kunaweza kutoa msukumo mkubwa wa kuwa na maendeleo endelevu, Jambo jingine lililotajwa ni kwamba watoto wanapaswa kutizamwakamawadau muhimu wa maendeleo ya dunia, hivyo wao ndiyo sehemu muhimu ambao wanaweza kuanguka kimaendeleo ama kufaulu.

Taarifa hiyo ya UNICEF imeanisha kile kinachopaswa kufanywa sasa ikiwemo pia kuwashirikisha watoto walioko kwenye maeneo ya pembezoni. Imearifiwa kwamba kiasi cha watoto milioni 165 walioko chini ya umri wa miaka mitano duniani kote wanakabiliwa na matatizo ya kudumaa, hali ambayo inaathiri ukuaji wa ubongo wao.