Mkutano kuhusu hatma ya miji waanza huko Sweden

24 Juni 2013

Huko Stockholm, Sweden wasomi, wataalamu wa makazim, watunga sera na wahusika wa maeneo ya umma wanakutana ili kujadili hatma ya maeneo hayo wakati huu ambapo ukuaji wa miji unashindwa kwenda sambamba na utoaji huduma za msingi kwa wakazi wake. Mkutano huo umendaliwa na shirika la makazi ya watu la Umoja wa Mataifa, UN-HABITAT kama anavyoripoti Jason Nyakundi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Mkutano huo ni matokeo ya jitihada za pamoja kati ya mradi wa vuguvugu la Ax:son Johnson na Shirika la makaazi la Umoja wa Mataifa UN- Habitat. Tangu jadi ukuaji wa miji umeonekana kuwa tatizo. Lakini hata hivyo  tatizo si ukuaji wa haraka wa miji bali kutokuwepo na uwezo  wa miji wa kustahilimi ukuaji na kutumia kwa njia inayofaa nafasi iliyopo na mali asili  kwa maendeleo mijini. Mkutano huo  wa hali ya baadaye ya maeneo ya umma ni sehemu ya mikutano mitatu ambayo itaandaliwa kila mwaka hadi mwaka 2016. Lengo la mkutano huu la ni kuleta maeneo ya umma kwenye mjadala. Mkutano huo pia utajadili umuhimu wa kuhusiha maoni ya watu na kuzuia  matatizo yanayoshuhudiwa wakatai wa kupanuka kwa miji. Kati yale yanayohitaji kuangaziwa ni pamoja ya miradi inayohusu mabomba jambo ambalo litazungumziwa kwa kina kwenye mkutano huo.