Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yasema chakula na lishe bora ni kipaumbele kwa Paksitani

WFP yasema chakula na lishe bora ni kipaumbele kwa Paksitani

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, Ertharin Cousin amehitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Pakistani ambapo ametaka jitihada mpya za kushughulikia suala la chakula na lishe nchini humo miongoni mwa watu wanaokabiliwa na ukimbizi wa ndani, majanga ya asili na umaskini. Taarifa ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.

(Taarifa ya Assumpta)

Bi. Cousin baada ya kutembelea miradi ya WFP huko Mingora na Kalam yenye lengo la kuhakikisha lishe bora kwa waathirika wa ukimbizi wa ndani na majanga ya asili alisema bayana kuwa Pakistani ikiwa ni nchi y enye rasilimali wananchi wake bado wanahaha kukidhi mahitaji ya kila siku kutkana na majanga kama vile mizozo ya kikabili kwenye ukanda wa kikabila unaosimamiwa na serikali kuu, FATA. Katika eneo hilo, WFP inatoa mgao wa dharura wa chakula kwa watu wapatao Milioni Moja. Halikadhalika WFP inatoa mlo maalum wenye virutubisho kwa wanawake wazazi Milioni moja na watoto wadodo kwa lengo la kuboresha afya zao. Mkurugenzi Mtendaji huyo wa WFP amesisitiza kuwa shirika lake litaendelea kusaidiana na nchi hiyo ili kufikia lengo la kutokomeza ukosefu wa uhakika wa chakula pamoja na unyafuzi au utapiamlo uliokithiri. Hadi mwishoni mwa mwaka huu WFP itahitaji dola Milioni 40 ili kutekeleza ipasavyo operesheni zake huko Paksitani.