Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha hatua ya Albania kuwapatia makazi raia wa Iraq

UM wakaribisha hatua ya Albania kuwapatia makazi raia wa Iraq

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq amekaribisha hatua ya kupewa makazi upya huko Albania kwa raia 27 wa Iraq waliokuwa wakiishi katika kambi moja iliyoko karibu na mji wa Baghdad.Hadi sasa kiasi cha watu 71 wanaarifiwa kuwasili salama huko Albania na tayari wameenza kunufaika na misaada inayoendelewa kutolewa na serikali nchini humo.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Martin Kobler amepongeza hatua hiyo akisema kuwa imefungua njia kwa raia wengi ambao walikuwa wakiishi katika mazingira ya kihoro.

Bwana  Kobler  ameongeza kusema kuwa pamoja na Albania, Ujerumani nayo imehaidi kuwapokea wakazi wengine 100 kwa ajili ya kuwatengea maeneo maalumu.