Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na shambulio dhidi ya watalii huko Pakistani

Ban asikitishwa na shambulio dhidi ya watalii huko Pakistani

Ripoti ya kwamba kundi la wapanda mlima wa kigeni walishambuliwa na kuuawa huko Kaskazini mwa Pakistani zimemsikitisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ambaye pamoja na kutuma salamu za rambi rambi kwa wafiwa, ameonyesha wasiwasi wake juu ya ongezeko la mashambulio ya kigaidi nchini humo.Bwana Ban amesema katika wiki chache zilizopita pekee, makumi ya raia wamepoteza maisha. Huku akisisitiza utayari wa Umoja wa Mataifa wa kuendelea kusaidia Pakistani kukabiliana na ugaidi, ameitaka serikali ya nchi hiyo kuchukua hatua za haraka kuwafikisha watuhumiwa mbele ya sheria na kuhakikisha usalama.