Hali ya ukosefu wa chakula yazidi kushuhudiwa huko Palestina: WFP/UNRWA

21 Juni 2013

Wakuu wa mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa hii leo wameelezea hisia zao kutokana na kuendelea kushuhudiwa uhaba wa chakula katika ukingo wa magharibi wa mto Jordan na Gaza ambapo moja kati ya familia tatu za wapalestina zinakabiliwa ugumu wa kulisha familia zao. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Ertharin Cousin Mkurugenzi mkuu wa Shirika la mpango wa chakula duniani WFP na Filippo Grandi ambaye ni kamishina mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA walitembela kijiji cha Bedouin kati ya ya mji wa Jerusalem na Jericho ambapo shughuli ya pamoja ya mashirika hayo ya usambazaji wa chakula ilikuwa ikiendelea. Bi. Cousin anasema kuwa bei ya juu ya vyakula na mishahara midogo ina maana kuwa wapalestina milioni 1.6 hawajui vile watapata chakula akionngeza kuwa usalama wa chakula ni muhimu katika kuhakikisha kuwepo kwa amani eneo hilo. Kulingna na utafiti wa Umoja wa Mataifa uliondeshwa na kituo cha takwimu kwenye utawala wa Palestina kwa ushirikiano na WFP,UNRWA na FAO umebaini kuwa watu milioni 1.6 au asilimia 34 ya familia hawana usalama wa chakula. WFP inawafikia takriban watu 650 wasio na chakula kweneye utawala wa palestina huku UNRWA ikiwapa msaada wa chakula zaidi ya wakimbizi wa kipalestina milioni moja kwenye eneo la mashariki ya kati.