UNICEF yaonya juu ya hali mbaya ya usafi kwa wakimbizi wa ndani Syria

21 Juni 2013

Zaidi ya watoto milioni 4 walioathirika na machafuko yaSyriawako katika hatari ya kupata maradhi ya kuambukiza kama kuhara kutokana na ukosefu wa majisafina vyoo limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Alice Kariuki na maelezo zaidi

(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)

Shirika hilo linasema wakimbizi wengi wa ndani wa Syria na wale wanaoishi katika makambi ya wakimbizi nchi jirani wako katika hatihati ya kupata matatizo makubwa ya upungufu wa maji katika miezi ijayo ya majira ya joto. Marixie Mercado kutoka UNICEF anasema familia nyingi za wakimbizi wa ndani na wakimbizi wengine wanaishi kwenye makambi yaliyofurika watu ambako kuzingatia usafi ni tatizo kubwa akiongeza kwamba hali huenda ikawa mbaya zaidi kutokana na ongezeko la joto.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)

“UNICEF inaonya kwamba kupanda kwa kiwango cha joto, mrundikano wa watu na hali mbaya ya usafi ni matishio ya karibuni yanayowakabili watoto milioni 4 walioathirika na vita vinavyoendelea Syria na kwamba bila maji salama ya kutosha na usafi uwezekano wa watoto kuugua kuhara na maradhi mengine utaongezeka. Wakati vita vikisababisha watu wengi kukimbia UNICEF inaongeza juhudi za kutoa maji salama na huduma za usafi ikiwafikia watu milioni 9 tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Syria jenereta mpya na kukarabatiwa kwa mfumo wa maji kumesaidia mfumo wa maji na mitambo ya kusafisha maji kuendelea kufanya kazi hata katika maeneo ambayo yanamapigano makali. Jordan UNICEF na washirika wake wanaingiza lita milioni 4 za maji kila siku kwenye kambi na Zaatari wakati wakikarabati mitambo mingine na miundombinu katika miji ya jirani. Mitambo ya maji pia imewekwa kwenye kambi mpya ya Azraq. Lebanon UNICEF na washirika wake wamegawa vifaa vya usafi wa watu zaidi ya 430,000.”

 UNICEF inasema inahitaji dola milioni 200 kutoa msaada wa maji na huduma za usafi kwa familia za wakimbizi wa ndaniSyriana waliokimbiliaJordan,LebanonnaIraq. Hadi sasa imefanikiwa kuchangisha dola milioni 76 ili kutoa huduma hizo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter