Njaa katika dunia iliyojaaliwa ni kashifa:Papa Francis/FAO

20 Juni 2013

Baba mtakatifu Francis amewataka washiriki kwenye mkutano wa 38 wa shirika la chakula na kilimo FAO kushirikiana kwa pamoja kupiga vita njaa, lakini pia kuchukua hatua zaidi ya tofauti zao katika sera ambazo hazijumuishia wanyonge na zinazochangia njaa na umasikini duniani. Akizungumza alipokutana na washiriki hao mjini Vatcan amesema ukweli ulio bayana kwamba kiwango cha uzalishaji hivi sasa kinatosheleza, lakini mamilioni ya watu bado wanataabika na kufa na njaa, hii ni kashifa.

Papa amepokea ujumbe wa washiriki hao kutoka kila kanda ya duniani ikiwa ni katika kuendeleza utamaduni ulioanza miaka 60 iliyopita. Papa pia amelishukuru na kulipongeza shirika la FAO kwa kazi zake.

Papa Francis amesema mdororo wa uchumi hauwezi kuendelea kutumikakama kisingizio na hauwezi kuisha hadi pale hali ya maisha itakapopigwa darubini kwa kina na kwa kuzingatia utu.

Ameonya kuwa utu wa watu uko hatarini kwa kukabiliwa na masuala kama matumizi ya nguvu, vita, utapia mlo, wengine kusahaulika, ukiukwahi wa haki, na utabiri wa masuala ya fedha ambao sasa unaathiri bei za chakula.