Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lapongeza makubaliano ya Mali

Baraza la Usalama lapongeza makubaliano ya Mali

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limesema kuwa hatua ya kusainiwa makubaliano ya Ouagadougou ambayo yanaweka uwanja wa kuelekea kwenye uchaguzi wa rais na kuanzishwa kwa duru la mazungumzo ya amani baina ya serikali ya mpito na kundi la vugu vugu la kitaifa kwa ajili ya mali ,MNLA ni hatua inayopaswa kupongezwa.

Baraza hilo limesema kuwa kitendo hicho kinamaanisha kuwa pande zote kwenye mzozo huo zimeazimia kujenga utaifa, haki ya kimipaka na kuleta umoja wa kitaifa miongoni mwa raia wa Mali.

Kadhalika baraza hilo limepongeza juhudi za usuluhishi zinazoendeshwa na Jumuiya ya za nchi zilizoko Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) chini ya uongozi wa rais wa Burkina Faso anayesaidiwa na rais wa Nigeria. Umoja wa Mataifa pia umeweka mwakilishi wake kwenye majadiliano hayo.