Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM, OIC na serikali ya Ufilipino washirikiana kuwasaidia watu nchini Ufilipino

UM, OIC na serikali ya Ufilipino washirikiana kuwasaidia watu nchini Ufilipino

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa ukiongozwa na serikali ya Ufilipino, muungano wa kislamu OIC , Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA na mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Ufilipino unakamilisha ziara yake hii leo. Ziara hiyo ilitoa fursa ya kutoa hamasisho kuhusu hali ya kibinadamu nchini Ufilipino , majukumu ya shughuli za kibinadamu kusadia mahitaji ya kibinadamu na kuonyesha umuhimu wa kujiandaa kwa majanga yanayojirudia.

Ujumbe huo pia ulitembela jamii zinazofaidika na progamu hizo kupitia kwa mipangilio ya serikali ya kuleta mandeleo kwenye sehemu zinazokumbwa na mizozo. Mkurugenzi mkuu wa OCHA Rashid Khalikov anasema kuwa jamii ya kimataifa ni lazima itoe msaada kwa serikali kuhakikisha kuwa watu walioathiriwa wana matumani ya siku za baadaye.