Ukatili wa kingono dhidi ya wanawake ni tatizo la afya ya jamii duniani: WHO

20 Juni 2013

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani WHO na washirika wake imedhihirisha kuwa ukatili wa kingono au kimwili dhidi ya wanawake ni tatizo la afya ya jamii duniani ambalo huathiri zaidi ya theluthi moja ya wanawake duniani kote. George Njogopa anafafanua zaidi.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Ikichambua mazingira ya wanawake kunyanyaswa, ripoti hiyo inasema kuwa matukio mengi ya unyanyasaji huo hujitokeza ndani ya maisha ya wenza na vingine hujitokeza katika mazingira ya kawaida.

Lakini katika hali isiyo ya kawaida, ripoti hiyo imeweza kueleza vitendo vya unyanyasa anavyokumbana na mwanamke aliye nje ya maisha ya mahusiano ya kimapenzi.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa zaidi ya asilimia 35 ya wanawake wanakumbana na vitendo vya unyanyasaji bila kujali kuwa wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi na wenzao wao ama nje ya mahusiano hayo.

Kwa upande mwingine  utafiti huo umenyesha kuwa asilimia 38 ya wanawake duniani kote waliuwawa na wapenzi zao wakati asilimia 42 ya wanawake walikumbana na vitisho na vitendo vya unyanyasaji ikiwemo kujeruhiwa.

Dr  Naeemah Abrahams kutoka baraza la utafiti tiba anaeleza namna ripoti hiyo inavyohusika kwa Afrika.

(SAUTI YA Dkt. Abrahams)