Dola Milioni 485 zahitajika kwa usaidizi wa kibinadamu huko Juba

20 Juni 2013

Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yaliyoko Sudan Kusini yanahitaji dola Milioni 485 hadi mwishoni mwa mwaka huu , ili kusaidia watu Milioni Tatu huko Juba kuweza kujenga upya maisha yao. Hiyo ni kwa kwa mujibu wa ripoti ya tathmini ya kati ya mwaka operesheni kubwa zaidi ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi wa binadamu barani Afrika . Jason Nyakundi na taarifa zaidi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Wakishirikiana kwa karibu na wizara ya masusla ya kibinadamu na majanga, mashirika ya Umoja wa Mataifa na yale yasiyokuwa ya serikali  yametekeleza karibu asilimia 90 ya majukumu yao kwa kipindi cha miezi sita ya mwaka huu hata kama yanahudumu kwenye moja ya mazingira magumu zaidi duniani. Mratibu wa masusla ya kibinadamu nchini Sudan Kusini Toby Lanzer anasema kuwa

hatakamamaisha ya jamii nyingi nchini Sudan Kusini yalionekana  kuboreka miezi ya kwanza kutokana na kuwepo kwa mavuno mazuri hata hivyo ghasia zimesababisha kuhama kwa maefu ya watu kwenye maeneo ya Jonglei. Hata kama utafiti unaonyesha kupungua kwa mahitaji kutoka dola bilioni 1.16 hadi dola bilioni 1.05 hadi mwezi Juni  wahisani wametoa hadi sasa dola milioni 567 kukiwa na pengo la dola milioni 485.