Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulio la Moghadishu ni unyama usiokubalika:Ban

Shambulio la Moghadishu ni unyama usiokubalika:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio la Jumatano kwenye ofisi za Umoja wa mataifa mjini Moghadishu na kuliita ni unyama na ukatuili usioelezeka. Ameyasema hayo akiwa mjini Beijingwakati wa mkutano wake na waziri wa mambo ya nje wa Uchina Yang Jiechi. Ban ametoa pole kwa familia za wahanga na kuwatakia nafuu ya haraka majeruhi. Amesema mashambulio kama hayo hayakubaliki hasa ukizingatia kuwa Umoja wa mataifa uko hapo kuwasaidia watu waSomalia, kuwapa maendeleo, kuwapa msaada, kuhakikisha utulivu wa kisiasa na kuchagiza haki za binadamu na utu.