Mahitaji ya wakimbizi kote ulimwenguni yanapaswa kuzingatiwa:WFP

19 Juni 2013

Kwa zaidi ya miaka miwili, ulimwengu umeshuhudia mamailioni ya wasyria wakikimbia  makwao, kukimbia ghasia huku wakitafuata usalama, na hiyo ni kauli ya Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP katika kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani juni 20. George Njogopa na taarifa kamili.(TAARIFA YA GEORGE)

Familia nyingi zimejikuta zikilazimika kuhama zaidi ya mara moja huku zikiwa mikoni mitupu mbali ya kubebe kile kinachowezekana kubebeka.

Madhira yanayowakuta wananchi hao kutokana na mapigano yanayoendelea kuchacha nchiniSyriani makubwa, na wakati mwingine ni vigumu mno kuyatolea jambo la kufananishia.

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa kutokana na hali inavyoendelea nchini humo, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu litakakuwa limetoa msaada wa chakula kwa watu zaidi ya milioni saba, wengi wao wakiwa ni wakimbizi wa ndani na wengine waliokwenda kuomba hifadhi ya kikimbizi katika nchi za jirani.

Kuna hali ya sintofahamu inayoendelea kuwakumba raia waSyriabila kujalisha wale walioko ndani ya nchi  ama wale wanakimbilia nchi za mbali, lakini ukweli wa mambo taifahilolipo kwenye kipindi kigumu.