UNAIDS na Lancet kuangazia mjadala wa afya ulimwenguni baada ya 2015

19 Juni 2013

Katika kuhakikisha ajenda ya afya inaangaziwa ipasavyo baada ya ukomo wa malengo ya  maendeleo ya milenia 2015. Shirika la umoja wa mataifa linalohusika na maswala ya ukimwi UNAIDS na lancet, limetangaza majina ya makamishna ambao watakua wakishirikiana katika suala la ugonjwa wa virusi vya ukimwi na afya kwa ujumla Alice Kariuki anaripoti.(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Zaidi ya makamishna 30 , wakiwemo wakuu wan chi, watunga sera, watu wanaoishi na virusi vya ukimwi, wataalamu na vijana chipukizi wanatazamiwa kukutana kwa siku mbiliLilongwe,Malawikwa ajili ya kujadilia njia bora zaidi za kukabiliana na tatizo la ukimwi kwa ajili ya kuokoa kizazi cha siku za usoni.

Kongamanohiloambalo ni la kwanza  kufanyika nchiniMalawi, limepangwa kuanza Juni 28 hadi 29 .

Akizungumzia kongamanohilo,Mkurugenzi Mkuu wa UNAIDS, Michel  Sidibe amesema kuwa hii ni fursa adimu ambayo inawakutanisha watu kutoka kariba mbalimbali kwa ajili ya kujadilia mbinu za kukabiliana na tatizo la UKIMWI.

Rais wa Malawi Joyce Banda anatazamiwa kuwa mwenyekiti wa kongamanohiloatayesaidiana na Mwenyekiti wa Kamishna ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini Zuma na Mkurugenzi waLondonSchool of Hygiene and Tropical Medicine Peter Piot.