Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

AMISOM yalaani mashambulizi kwenye makao ya UM nchini Somalia

AMISOM yalaani mashambulizi kwenye makao ya UM nchini Somalia

Mjumbe maalum wa mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika nchini Somalia balozi Mahamat Saleh Annadif amekashifu vikali shambuli la kigaidi la hii leo kwenye makao ya Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu shambulizi linaloaminika kuendeshwa na wanamgambo wa Al- Shabaab. Balozi Mahamat amepongeza hatua za haraka za kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika AMISOM na vikosi vya Somalia akisisitiza kuwa AMISOM itafanya kila jitihada kuleta udhabiti nchini Somalia.

Amesena kuwa mashambulizi yanayoendeshwa na Al- Shabaab yanalenga kusambaratisha jitihada zinazoendeshwa na watu wa Somalia za kujimwamua kutoka kwenye ghasia akiongeza kuwa mashambuzi hayo hayawezi jitihada za kuendelea kuwaunga mkono watu wa Somalia kuijenga upya nchi yao.