Mwakilishi wa UM Somalia alaani shambulio dhidi ya UM Moghadishu:

19 Juni 2013

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa nchiniSomaliana mkuu wa UNSOM Nicholas Kay amelaani vikali shambulio dhidi ya maskani ya Umoja wa Mataifa mjini Moghadishu.Mapema leo asubuhi marira ya saa 11:30 saa zaSomaliapickup iliyosheheni mabomu ililipuka kwenye lango kuu la maskani ya Umoja wa Mataifa na washambuliaji wakaingia kwa mkuu katika ofisi hizo.

 Majibishano ya risasi na milipuko mingine ikafuata wakati wafanyakazi wa wakihaha kujificha penye usalama.

Bwana Kay amesema ameshtushwa saana tukiohilola leo mjini Moghadishu. Eneo lililoshambuliwa ni ofisi za wafanyakazi wa wa Umoja wa Mataifa wa huduma za kibinadamu na maendeleo kwa ajili ya watu waSomalia.

Pia ameushukuru mpango wa Muungano wa Afrika wa kulinda amani AMISOM ambao ulifika mara moja na kuwalinda wafanyakazi wa Umoja wa mataifa wa Kisomali na wale wa Kimataifa. Watu kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa katika shambuliohilo.