Mamilioni ya watu walazimika kuhama makwao mwaka 2012:UNHCR

19 Juni 2013

Zaidi ya watu milioni 7.6 walilazimika kuhama makwao mwaka 2012 kwa mujibu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

UNHCR inasema kuwa watu milioni 1.1 walilazima kuhama mataifayaokama wakimbizi huku watu milioni 6.5 wakilazimika kuwa wakimbizi wa ndani, ndani ya nchi zao.

UNHCR inasema kuwa kasi ya watu kuhama makwao mwaka wa 2012 ilikuwa ya juu zaidi kwa kipindi cha miaka ishirini iliyopita. Vita vinasalia kuwa sababu kuu ya watu kuhama wakati asilimia 55 ya wakimbizi wote wakiwa wanatoka kwenye mataifa yaliyoathiriwa na mapigano yakiwemoAfghanistan,Somalia ,Iraq,Syria naSudan. Mkuu wa UNHCR Antonio Gutteres anasema kuwa kuongezeka kwa watu wanaohama ni ishara ya changamoto zinazoikumba jamii ya kimataifa katika kutatua mizozo.

 (CLIP YA ANTONIO GUTERRES)

"Asilimia 87 ya wakimbizi duniani wanalindwa na nchi kwenye ulimwengu unaoendelea. Kwa hivyo wakati tunaona mazungumzo kuhusu wakimbizi kwenye nchi zilizostawi  nafikiri ni vizuri kuwakumbusha kuwa wakimbizi si watu  wanokimbia nchi maskini na kuingia nchi tajiri kutafuta maisha bora hapana. Wakimbizi ni watu ni watu waliokimbia kwa sababu walilazimishwa na wengi wao wanaishi kwenye nchi maskini  zaidi duniani. Mwaka 2012 ulikuwa na karibu wakimbizi 650,000 waliokimbia mzozo nchini nSyria. Kwa sasa tuna zaidi ya wakimbizi milioni 1.6 maana kuwa idadi ya wakimbzi walioikimbia Syria tangu mwanzo wa mwezi Januari ni zaidi au sawa na idadi ya wakimbizi wote waliohama makwao duniani kote mwaka 2012. Hii inakupa picha jinsi hali nchini Syria ilivyo."

Bwana Guterres anasema kuwa karibu nusu ya wakimbizi wote ni watoto walio chini ya miaka 18.