Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha kutiwa saini mkataba wa amani Mali

Ban akaribisha kutiwa saini mkataba wa amani Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha kusainiwa kwa mktaba wa amani baina ya serikali ya Mali, Kundi la Azawad na Baraza la Umoja wa Azawad leo Juni 18 mjini Ouagadougou, Burkina Faso.

Miongoni mwa vipengee vya mkataba huo, ni kutaka mapigano yasitishwe mara moja, kuweka njia ya kufanya uchaguzi wa urais kote nchini na pande zote kuahidi kujadili amani ya kudumu nchini Mali kupitia mazungumzo jumuishi yatakayofanyika baada ya uchaguzi.

Bwana Ban ametiwa moyo na pande zote kuahidi kuunga mkono maridhiano ya kitaifa, na kusuluhisha mizozo kwa njia ya amani. Amezitolea mwito zianze kuutekeleza mkataba huo mara moja. Ameishukuru jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, kwa juhudi zake za upatanishi, chini ya uongozi wa Rais  Blaise Compaoré wa Burkina Fasona na Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria.